Jumatatu, 13 Mei 2013

TAMASHA LA DIAMOND JIJINI BUJUMBURA LA FANA

Msanii wa Bongo Fleva Nasib Abdoul almaharufu kama Diamond amewaburudisha wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jijini Bujumbura  ambapo watu kutoka katika kata mbalimbali za manispaa ya jiji hilo walijitokeza kwa wingi kushudia tamsha hilo lililofanyika kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika kwenye ukumbi wa Hotel Cocktail Beach.
Watu kutoka katika tarafa za Buyenzi, Bwiza, Jabe, Nyakabiga, Kamenge, Musaga, Kinama, Cibitoke, Kanyosha, Kibenga walimiminika kwa wingi katika eneo hilo. habari zaidi ni kwamba kuna hata wapenzi wa muziki kutoka Uvira nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo DRCongo ambao hawakuridhika na tamasha la hapo Uvira la siku ya Jumamosi na kujiunga na Warundi hapo Cocktail Beach.
Picha ya Diamond na msanii wa Burundi Lolilo

Diamond ambae alikuwa ameshuka katika ukanda huo wa maziwa makuu na kundi lake la Wasafi classic kutoka jijini Dar Es Salaam Tanzania, na kufikia kwenye Hotel Club du Lac Tanganyika, moja miongoni mwa hoteli kubwa zenye mandhari nzuri jijini hapo.




DIAMOND ALIVYOKUWA CHINI YA ULINZI MKALI TARAFANI UVIRA/DRCONGO

Wapenzi wa muziki kutoka katika mitaa mbalimbali ya tarafa ya Uvira na Fizi, kule Kalimabenge, Kalundu, kilibula, Kiliba, Sange, Kavimvira, Kasenga na Mulongwe, walimiminika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa mpira wa miguu tarafani hapo Uvira kushuhudia tamasha la msanii wa bongo Fleva Nasib Abdoul almaharufu kama Diamond ambae amejizoolea umaharufu katika nchi za afrika mashariki na kati.

Shughuli za usafiri na biashara ziliparaganyika siku hiyo alipowasili tarafani Uvira akitokea nchini Burundi kupitia mpaka wa Gatumba na Kavimvira kwenye umbali wa kilometa 30 na mji  mkuu wa Burundi Bujumbura ambapo kila mtu alitaka amuone live msanii huyo.

Hali ya hewa ilichafuka pale baada ya tamasha watu waliokuwa wamefurika kwa wingi walijaribu kila mmoja kutaka kumsabahi na wengine angalau kutaka kumgusa, polisi na  Jeshi la FARDC  kama unavyoona kwenye picha hiyo, ililazimika kumlinda zaidi kuhakikisha kijana huyo anaendelea kuwa salama.